Wednesday, 26 September 2018

MTAALAM WA NYOTA ASEMA HAMISA HAWEZI KUMZIDI WEMA SEPETU

Akizungumza na Ijumaa Wikienda  mnajimu/mtaalamu wa nyota Maalim Hassan amesema watu ambao nyota yao ni mizani huwa wana asili ya kupendwa na watu ambapo nyota hiyo ndiyo aliyonayo Wema Sepetu. Alisema kwa upande wa nyota ya Hamisa Mobeto ambayo ni mshale huwa watu hao wanapendwa na watu wa mbali na siyo wa nyumbani kwake na nyota yake huwa na nguvu kwenye tukio fulani tofauti na mizani ambayo huwa na nguvu muda wote.
.
“Hata siku moja Hamisa hawezi kumzidi Wema kwa kupendwa na umaarufu kama wanavyosema huko mitandaoni kwa sababu nyota ya Wema ni kali, Wema nyota yake ni mizani na mizani kitaalam asili yake ni hewa na kama unavyojua hewa kila mahali ipo na kila sehemu inapenya yaani lazima atafahamika sana mtu mwenye nyota hii na atapewa thamani sehemu yoyote ile.
.
“Kwa upande wa Hamisa yeye nyota yake ni mshale ambayo asili yake ni moto na moto hauwezi kuwaka vyema bila hewa na ndiyo maana hata siku moja moto hauwezi kuizidi hewa nguvu kwa sababu moto siku zote unategemea hewa ndipo uwake vizuri na itabaki hivyo na ndiyo maana hata kwa upande wa nguvu kinyota, hewa ina nguvu zaidi,” alisema mtabiri huyo na kuongeza
.
“Kwa hiyo Hamisa anaweza kupata umarufu sana akitoka nje ila siyo kwake kwa maana ya kwamba Hamisa anaweza kupendwa zaidi nje ya nchi kuliko Tanzania kwa sababu mshale ukikaa sehemu moja hauna madhara ila ukiurusha kwenda mbali kule unakokwenda ndiyo kutakuwa na madhara. Hamisa hawezi kupata thamani akiwa hapa kama ambavyo atapata akiwa nje ila Wema yeye popote pale atapata thamani, kwa hiyo Hamisa hawezi kumzidi Wema" Alisema kwa mujibu wa GPL
.
Nini maoni yako?